RATIBA YA LIGI KUU BARA LEO

LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea leo ambapo mechi mbili zinatarajiwa kuchezwa ikiwa ni mzunguko wa nne.

Mbeya City wataikaribisha Azam FC kwenye mchezo wa ligi unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Azam FC imetoka kulazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 dhidi ya Yanga inakaribishwa na Mbeya City ambayo imecheza mechi tatu.

Mchezo wake wa mwisho kwenye ligi wa mzunguko wa tatu iliambulia sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Tanzania Prisons.

Yanga watawakaribisha Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa ligi unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Yanga imetoka kulazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 dhidi ya Azam FC na Mtibwa Sugar imetoka kushinda mabao 3-1 dhidi ya Ihefu.