ISHU YA KISINDA NA ONYANGO IMEGOTEA HAPA

BEKI Joash Onyango anatajwa kubaki Simba SC mpaka mkataba wake utakapogota mwisho huku Tuisila Kisinda wa Yanga akitajwa kuwa nafasi yake itakuwa ndani ya kikosi hicho mpaka dirisha dogo.

Mashauriano ya wachezaji haya yalikuwa yanasikilizwa na Kamati ya Sheria, Wanachama na Hadhi za Wachezaji ambapo Kisinda yeye alisajiliwa muda mfupi kabla dirisha la usajili kufungwa huku taarifa zikieleza kuwa tayari Yanga ilikuwa imeshakamilisha idadi ya wachezaji wakigeni 12.

Onyango yeye mkataba wake na Simba ni dili la miaka miwili lakini aliomba kuvunjiwa mkataba hapo ili apate changamoto mpya.

Kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi amesema kuwa wameomba TFF imtoe Joyce Lomalisa ili asajiliwe Kisinda hivyo wanasubiri.

Kuhusu Onyango, Meneja wa Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally alisema kuwa Onyango bado ana mkataba na Simba wa miaka miwili.