JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Simba amesema wananafasi kubwa ya kushinda kwenye mchezo dhidi ya Big Bullets ambao ni wa Ligi ya Mabingwa Afrika unaotarajiwa kuchezwa nchini Malawi.
Mchezo wa leo unakuwa ni wa kwanza kwa Mgunda kukaa benchi baada ya kuibuka ndani ya Simba akitokea Klau ya Coastal Union.
“Tunajua kwamba mchezo wetu utakuwa mgumu na tupo tayari tutajitahidi kupata matokeo kwenye mchezo wetu.
“Mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi na kutuombea kwani tunatambua kila mmoja anahitaji kuona tunapata ushindi.
“Sijakaa muda mrefu na timu ila nitashirikiana na benchi la ufundi ambalo nimelikuta tunaamini kila kitu kitakuwa sawa,” amesema.
Jana Simba imefanya mazoezi ya mwisho kwa ajili ya mchezo wa leo na miongoni mwa wachezaji ambao walikuwa kwenye mazoezi ni Jonas Mkude, Sadio Kanoute na Clatous Chama.