SHABIKI WA SIMBA ASHINDA MAMILIONI YA M BET

SHABIKI wa Klabu ya Simba anayeishi mkoani Arusha, Joseph Marwa ameshinda sh 60, 321,350 baada ya kubashiri kwa usahihi mechi 12 za ligi mbalimbali duniani kupitia mchezo wa Perfect 12 wa kampuni ya M-Bet.

Marwa ambaye ni mjasiriamali amesema kuwa awali hakuwa na imani na michezo ya kubashiri kabisa mpaka alipofuatwa kukopwa fedha ya nauli  na mmoja wa washindi kampuni ya M-bet.

Amesema kuwa mshindi huyo alimfuata kumkopa nauli ya kwenda Dar es Salaam na kuahidi angemrudishia mara baada ya kupokea fedha alizoshinda.

Alifafanua kuwa kwa vile pamoja na kumfahamu mshindi, bado alikuwa anasita kumkopesha kwani kipindi hicho hakuwa na imani na michezo ya kubashiri.

“Nilimpa Sh150,000 mshindi na rafiki yake ambao walikuja Dar es Salaam kufuata fedha hizo. Sikuwafuatilia  kabisa sababu walikuwa vijana ninao wafahamu, lakini mara baada ya kurejea, kijiana alinirejeshea fedha yangu na kwa kuongeza Sh 50,000 zaidi.

“Sikuamini kabisa na kuanza kumhoji maswali kadhaa na baadaye kumuomba anifundishe kuweka mkeka. Alifanya hivyo na siku ya kwanza tu tokea kuanza kubashiri, nilishinda 800,000 na zaidi ambazo nilitumiwa kwenye simu.

“Tokea hapo nikaanza kubashiri na M-bet na kushinda fedha mbalimbali kabla ya kuibuka mshindi katika Jackpot,” amesema Marwa.

Marwa pia aliwapa rai vijana wenye umri kuanzia miaka 18 kutumia 1,000 kubashiri na M-bet na kujishindia mamilioni ya fedha kama yeye.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Masoko wa M-bet, Allen Mushi amesema kuwa Marwa anakuwa mmoja wa wanachama wa nyumba yao ya mabingwa kwani ni mshindi wa tisa wa Jackpo tokea kuanza mwaka huu.

“Tunaposema M-bet ni nyumba ya mabingwa tunakuwa na maana maalum, mpaka sasa tumewazadia mamilioni washindi nane na wameweza kubadili maisha yao,” amesema Mushi.