AZAM FC licha ya kutangulia kuanza kufunga mbele ya Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Mkapa walikwama kusepa na pointi tatu jumlajumla.
Ikiwa chini ya Kali Ongala, ambaye ni kocha wa washambuliaji walianza kupachika bao la kuongoza kupitia kwa Daniel Amoah dakika ya 25 kisha Yanga wakafunga bao la kusawazisha kupitia kwa Feisal Salum dakika ya 57.
Bao la pili kwa Azam FC limefungwa na Malicous Ndoye dakika ya 65 kisha Fei dakika ya 77 akasawazisha kwa mara nyingine na kufanya ubao usome Yanga 2-2 Azam FC.
Yanga inafikisha pointi 7 kibindoni baada ya kucheza mechi tatu na sare moja na ushindi kwenye mechi mbili huku Azam FC ikifikisha pointi tano ina sare mbili na ushindi kwenye mchezo mmoja.
Katika mchezo wa leo, Yanga walikosa penalti iliyopigwa na Djuma Shaban baada ya kipa Alhamada kuiokoa.