>

GEITA V KAGERA SUGAR KUWAONA NI BUKU TATU

KUWAONA matajiri wa dhahabu, Geita Gold wakisaka pointi tatu dhidi ya Kagera Sugar ni buku tatu, (3,000) kwa mzunguko.

Ni mchezo wa ligi ikiwa ni mzunguko wa tatu kwa timu hizo ambazo ziashiriki Ligi Kuu Bara msimu wa 2022/23.

Kwa upande wa VIP B kiingilio ni 5,000 na kwa upande wa VIP A kiingilio ni 10,000.

Kagera Sugar ilipoteza kwenye mechi zake mbili ilizocheza msimu huu kwa kuanza na kupokea kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Azam FC na ikapoteza kwa kufungwa mabao 3-0 dhidi ya Simba.

Geita Gold wao walianza kupoteza kwa kufungwa mabao 3-0 dhidi ya Simba na sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Azam FC.