SIMBA KUCHEZA MWINGINE WA KIMATAIFA

BAADA ya kurejea kutoka nchini Sudan kikosi cha Simba kesho kinatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya AS Arta Solar, Uwanja wa Mkapa.

 

Simba ilialikwa kwenye michuano maalumu iliyoandaliwa na Al Hilal ambapo iliweza kucheza mechi mbili za kirafiki.

Mchezo wa kwanza Kocha Mkuu wa Simba, Zoran Maki alishuhudia timu hiyo ikishinda mabao 4-2 dhidi ya Asante Kotoko na ule wa pili ilipoteza kwakufungwa bao 1-0 dhidi ya wenyeji Al Hilal.

Seleman Matola, Kocha Msaidizi wa Simba amesema kuwa mechi hizo ni maalumu kwa ajili ya kufanya maandalizi yao kimataifa na wanaamini kwamba watafanya vizuri.

“Mechi zetu za kimataifa ilikuwa ni kipimo kizuri kwa ajili ya mechi zetu za kimataifa na tunaamini kwamba tutakwenda kufanya vizuri,”.

Mchezo ujao wa kwenye ligi ni dhidi ya KMC unaotarajiwa kuchezwa Septemba 7 Uwanja wa Mkapa na ule wa kimataifa ni dhidi ya Big Bullets unaotarajiwa kuchezwa Septemba 10 Simba ikiwa ugenini katika mchezo huu wa awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika.