SAFU YA USHAMBULIAJI YA SIMBA KAZI KWELIKWELI

 NAHODHA wa Simba, John Bocco msimu wa 2022/23 amecheza mchezo mmoja akitumia dakika 6, hajafunga bao wala kutoa pasi chini ya Kocha Mkuu, Zoran Maki.

Mbali na Bocco, rekodi za washambuliaji wa kikosi cha Simba kwa msimu huu hazijawa bora kwa kuwa kwa nyota wote watano ni mmoja kafanikiwa kufunga mabao mawili.

Kibu Dennis mfungaji namba moja ndani ya Simba ambaye alifunga mabao 8 msimu wa 2021/22 msimu huu hajafunga bao hata moja.

Nyota mwingine ni Mzungu wa Simba, Dejan Georgijevic ambaye kwenye mechi tatu za mashindano ndani ya ardhi ya Tanzania amefunga bao moja.

Moses Phiri ni kinara kwa watupiaji ndani ya Simba akiwa ametupia mabao mawili kwenye mechi mbili ambazo amecheza.

Habib Kyombo kacheza mechi mbili hajafunga wala kutoa pasi ya bao hivyo Maki ana kazi ya kuwanoa washambuliaji wake hawa kuwa kwenye kasi kubwa.