MADILI yote ambayo yalikuwa yanatajwa juu yake mwisho yamezimwa na sasa ni rasmi mwaba Fiston Mayele bado yupo sana ndani ya Yanga.
Nyota huyo alikuwa anatajwa kuwa kwenye rada za timu kubwa Afrika ikiwa ni pamoja na Morocco, Afrika ya Kusini ambazo zilikuwa zinahitaji saini yake.
Yanga wameamua kumpa dili lingine ambalo litamfanya adumu hapo mpaka 2024 akiwatumikia chini ya Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.
Uwezo wake wa kufunga mabao unawafanya wengi kuvutiwa na uchezaji wake huku mtindo wa kutetema akifunga ukizidi kupasua anga kila kukichwa.
Baada ya kuongeza dili hilo Mayele amesema kuwa yupo ndani ya Yanga na anafurahia kuwatumikia Wananchi.