MCHEZO wa kwanza wa kirafiki nchini Sudan kwenye mashindano maalumu ambayo Simba kutoka Tanzania imealikwa na Al Hilal wameibuka na ushindi wa mabao 4-2 Asante Kotoko.
Kipa namba moja kwenye mchezo huo alikuwa Ally Salim ambaye alibeba mikoba ya Aishi Manula na Beno Kakolanya ambao wapo kwenye majukumu ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.
Ni mabao ya Agustin Okra dakika ya 19 ambaye aliweza kuweka usawa kwenye mchezo huo kwa kuwa Simba walianza kutunguliwa.
Pape Sakho alipachika bao moja dakika ya 26 huku mwamba Clatous Chama alitupia mabao mawili ilikuwa dakika ya 42 kwa mkwaju wa penalti na dakika ya 79.
Mabao ya Asante Kotoko yalipatikana kupitia kwa Mukala dakika ya 9 ambaye alikuwa wa kwanza kufunga na Amankona yeye alifunga bao dakika ya 79.
Seleman Matola, Kocha Msaidizi wa Simba amesema kuwa mashindano hayo yatawapa nguvu ya kufanya maandalizi mazuri kwenye mechi za ligi na za kimataifa.