KLABU ya Liverpool imeweka dau la pauni milioni 60 kuinasa saini ya kiungo wa Barcelona, Frenkie de Jong.
Mpango wa timu hiyo ni kuinasa saini ya nyota huyo ili aweze kutua ndani ya Anfield kwa ajili ya kucheza mechi za Ligi Kuu England pamoja na mashindano mengine.
Jurgen Klopp Kocha Mkuu wa Liverpool amebadili mawazo kuhusu kutaka kusajili kiungo mpya kabla ya dirisha la usajili kufungwa Septemba Mosi, mwaka huu 2022.
Klopp amesema:”Itakuwa vema kama tutafanikiwa kupata kiungo mpya, ni kweli mwanzo sikuwa na mpango wa kusajili kiungo, sikuwa sahihi ila sasa ninahitaji.
“Kwa hiyo tunataka kusaka kiungo kama timu tutafanya kitu sahihi kwa upande wetu, ” amesema.