UONGOZI wa Azam FC umefikia makubaliano ya kuachana na makocha wao wawili kwenye majukumu ya kuinoa timu hiyo hivyo watabadilishiwa majukumu.
Taarifa rasmi iliyotolewa na Azam FC imeeleza namna hii:”Tumefikia makubaliano ya pande mbili na kocha wetu, Abdihamid Moallin, na msaidizi wake, Omary Nasser, kuachia ngazi kama kocha mkuu na msaidizi mtawalia.
“Hata hivyo, makocha hao wataendelea kubaki kama sehemu ya idara ya ufundi klabuni kwetu katika nafasi nyingine ambazo tutazitangaza hapo baadaye.
“Kwa sasa timu itakuwa chini ya Daniel Cadena, ambaye ni kocha wa makipa, hadi tutakapotangaza kocha mpya.
“Cadena ni kocha mwenye leseni ya juu kabisa ya ukocha, UEFA Pro License,” .