SIMBA QUEENS MABINGWA KIMATAIFA

BAADA ya ubao wa Uwanja wa Azam Complex kusoma She Corporate 0-1 Simba Queens katika Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Wanawake ukanda wa CECAFA Simba wanatangazwa kuwa mabingwa wa mashindano hayo.

Bao pekee la ushindi kwa Simba lilijazwa kimiani na Vivian Corazona dakika ya 46 kwa mkwaju wa penalti.

Dakika 45 za mchezo wa leo hakuna timu ambayo iliweza kupata bao wala kadi nyekundu kwa mchezaji wa timu pinzani.

Ni Joel Bukuru kiungo msumbufu ndani ya uwanja mali ya Simba alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 44 kwenye mchezo wa leo kipindi cha kwanza na nyota wa She Corporate Cicc Nantango naye alionyeshwa kadi ya njano kipindi cha pili dakika ya 86.

Unakuwa ni ubingwa wa kwanza kwa Simba kuweza kuutwaa ikiwa ni rekodi kubwa kwa Tanzania.