BAADA ya Azam FC kukamilisha dakika 180 kwenye Ligi Kuu Bara na kusepa na pointi nne leo kikosi hicho kitakuwa Zanzibar.
Mchezo wa kwanza wa ligi Azam FC iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar na iliambulia sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Geita Gold.
Mechi zote hizo mbili zilichezwa Uwanja wa Azam Complex,saa 1:00 usiku.
Lei kikosi cha Azam FC kitacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Taifa Jang’ombe saa 2:15.
Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa kila kitu kinakwenda sawa na waanaamini mchezo huo ni kipimo kwa ajili ya kuendelea kuwa imara kwa mechi zijaz