MZEE WA KUCHETUA BM ZALI LAKE LIPO HAPA

KIUNGO mshambuliaji ndani ya kikosi cha Yanga, Bernard Morrison ana zali na Coastal Union akiwa na uzi wa timu mbili tofauti kwa kuwatungua bao lake la kwanza.

 Raia huyo wa Ghana, msimu wa 2021/22 alikuwa akivaa uzi wenye rangi nyekundu na nyeupe alipokuwa ndani ya kikosi cha Simba na msimu huu wa 2022/23 uzi wake ni njano na kijani akiwa ndani ya Yanga.

 Ikumbukwe kwamba msimu wa 2021/22 bao lake la kwanza alifunga mbele ya Coastal Union kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

 Ni mechi 12 alicheza alipokuwa Simba, alitumia dakika 699 na alifunga bao moja pekee mbele ya Coastal Union ilikuwa ni Aprili 7,2022 Simba iliposhinda mabao 2-1.

 Aliporejea kwa mara nyingine Yanga msimu wa 2022/22 bao lake la kwanza kwenye ligi ilikuw dhidi ya Coastal Union, mchezo uliochezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Agosti 20.

 Bao hilo alipachika dakika ya 4 akitumia pasi ya Jesus Moloko, waliposhinda mabao 2-0 na kusepa na pointi tatu mazima.

Yanga chini ya Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi kwenye mechi mbili imekusanya pointi sita ikiwa imetupia mabao manne na kufungwa bao moja.

Ipo sawa pointi na Simba ambayo imetupia mabao matano pamoja na Singida Big Stars ambayo imetupia mabao matatu.