TEPSI Evance, kiungo wa Klabu ya Azam FC amejumuishwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars ambacho kimeanza maandalizi kwa ajili ya mchezo dhidi ya Uganda wa kuwania kufuzu CHAN unaotarajiwa kuchezwa Agosti 28,2022.
Nyota huyo kwenye mechi mbili za ligi amefunga mabao mawili na kutoa pasi moja ya bao.
Stars imeingia kambini Agosti 21 kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Wachezaji wengine ambao wameanza maandalizi ya mchezo huo ni pamoja na Aishi Manula, Bakari Mwamnyeto, Beno Kakolanya, Kibwana Shomari.
Kim Poulsen, Kocha Mkuu wa Stars amesema kuwa muda ambao upo ni mdogo lakini wanapaswa kufanya maandalizi mazuri kupata ushindi.
“Tumepata muda wa kufanya maandalizi lakini ukiangalia kwa namna ratiba ilivyo ni muda mfupi na kazi yetu ni kutafuta ushindi.
“Tunapaswa kujitahidi ili kushinda, mchezo utakuwa mgumu na hilo wachezaji wanajua kwamba haitakuwa kazi nyepesi,” amesema.