WACHEZAJI STARS KAZI IPO KUIKABILI UGANDA

MAJINA ya wachezaji wa timu ya Taifa ikiwa ni kwa ajili ya maandalizi ya kujiandaa na mchezo wa kufuzu Kombe la Mataifa Afrika, (CHAN) dhidi ya Uganda yameshawekwa wazi.

Nyota 25 ambao wameitwa kazi yao kubwa ni kuweza kuipeperusha bendera ya Tanzania kimataifa ili waweze kupata matokeo chanya katika mchezo huo.

Imani kubwa ni kuona kwamba kila mmoja ambaye ameitwa kwenye timu ya Tanzania afanye kazi kwa kujituma bila kuchoka na inawezekana kupata matokeo.

Hakuna kazi nyepesi hasa ukizingatia kwamba Uganda ni moja ya timu bora na ina wachezaji wazuri kwenye mchezo huo ujao.

Kikubwa kwenye maandalizi ambayo yanatarajiwa kuanza kufanyika leo kila mchezaji kufuata maelekezo ambayo atapewa na benchi la ufundi.

Wale ambao wameitwa wanapaswa kujua wameaminiwa na benchi la ufundi yale makosa ya kinidhamu ambayo yalikuwa yanatokea zamani basi yasiwepo ili timu iweze kupata matokeo.

Kila mmoja anajua kwamba kinachohitajika ni matokeo mazuri na kushinda kunahitaji kujituma bila kuogopa kwenye mchezo ujao dhidi ya Uganda.

Watanzania wanapenda kuona timu inashinda lakini ushindi haujawahi kupatikana kwa wepesi bila kupambana katika mechi ndani ya dk 90.

Kila la kheri kwenye maandalizi na wale ambao hawajaitwa wanajukumu la kuweza kufanya kazi kubwa kwenye mechi zao ili waweze kuitwa.

Hakuna mwenye uhakika wa kuitwa kikosi cha Stars ikiwa hatafanya juhudi kwenye mechi ambazo anacheza katika ligi na mashindano mengine