Jitihada za Muingereza Anthony Joshua kunyakua tena mataji ya uzito wa juu yaliyounganishwa ya dunia yalimalizika kwa mafadhaiko huku Oleksandr Usyk akitoa matokeo mazuri na kushinda kwa uamuzi wa uliowagawanya waamuzi huko Jeddah, Saudi Arabia.
Katika pambano lililoitwa ‘Rage on the Red Sea’, Joshua aliyekuwa na ukakamavu, mwenye umri wa miaka 32, alionyesha nia ya kutaka kutwaa taji hilo – na alionekana kujiboresha kutoka kwa pambano lao la kwanza – lakini hakuweza kuendana na ustadi wa raia huyo wa Ukraine .
Majaji wawili waliamua pambano hilo kwa 115-113 na 116-112 wakimpa ushindi Usyk, huku jaji wa tatu akimpa mpinzani 115-113. Ingawa kulikuwa na raundi zenye ushindani, Usyk alistahili ushindi.