UBAO wa Uwanja wa Mkapa, baada ya dakika 90 kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kwa upande wa Wanawake, Simba imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali.
Ni mabao ya Vivian Aquino Corazone anayevaa uzi namba 4 dakika ya 15 huku Philomena Abakay yeye alitupia mabao mawili na uzi wake mgongoni ni namba 27.
Mshambuliaji mahiri wa Simba Queens, Opa Clement anayevaa jezi namba 9 mgongoni alipachika bao moja dk ya 32.
Pongezi Simba Queens kwa ushindi ambao mmeupata katika mchezo wa kimataifa