KIKOSI cha Yanga kimeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Coastal Union kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kwa mabao ya Bernard Morrison dk ya 4 na Fiston Mayele dk ya 67.
Mayele ametetema kwa mara nyingine kwenye mchezo wa leo ambao alianzia benchi na alichukua nafasi ya Makambo Heritier.
Mchezo wa leo ni wa pili kwa Yanga kushinda ikiwa ugenini kwa msimu huu wa 2022/23 ambapo mechi ya kwanza ilikuwa dhidi ya Polisi Tanzania.
Katika mchezo wa Polisi Tanzania, ubao wa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid uliweza kusoma Polisi Tanzania 1-2 Yanga.
Morrison amepachika bao la kwanza akiwa na Yanga baada ya kurejea kwenye kikosi hicho kwa kuwa msimu wa 2021/22 alikuwa ndani ya Simba.
Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze aliweza kuonyeshwa kadi ya njano kutokana na kile kilichoonekana kutoridhishwa na maamuzi kwenye mchezo huo.
Yanga inafikisha pointi sita baada ya kucheza mechi mbili za ligi na imefunga jumla ya mabao matatu ikiwa imeruhusu kufungwa bao moja.
Mchezo wa leo wachezaji wote wa Yanga walivaa vitambaa vyeusi mkononi pamoja na benchi la ufundi kwa ajili ya maombolezo ya mashabiki wa Yanga waliopata ajali na wengine kutangazwa kutangulia mbele za haki.