SIMBA YASHINDA 3-0 GEITA GOLD

ZORAN Maki,Kocha Mkuu wa Simba amesema ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Geita Gold walistahili kwa kuwa wachezaji walicheza kwa kujituma.

Mabao ya Simba kwenye mchezo wa leo Agosti 17 yamefungwa na Agustino Okra,Moses Phiri na Clatous Chama ambaye amefunga kwa mkwaju wa penalti.

Ushindi huo unaifanya iweze kufikisha pointi tatu na kuongoza ligi ikiwa na idadi kubwa ya mabao ya kufunga ikifuatiwa na Mbeya City ambayo imeshinda mabao 3-1 dhidi ya Dodoma Jiji.

Mchezo wa leo ni wa kwanza kwa Simba kwenye ligi ikiwa chini ya Maki.

“Tumeweza kushinda mchezo wetu wa leo ambao ulikuwa mgumu na kila mmoja ameona namna ambavyo Geita Gold walikuwa wakicheza hasa kwenye eneo la kiungo.

“Kikubwa ni kuona tumepata pointi na tunakazi ya kufanya kwa mechi zijazo ili kuweza kupata ushindi zaidi,” .