KANUNI MPYA ZA WACHEZAJI WAKIGENI KUANZA LEO

 BODI ya Ligi Kuu Tanzania Bara, (TPLB) imebadilisha kanuni baada ya kufanya kikao cha maboresho ya kanuni za Ligi Kuu Bara.

Kikao cha Kamati ya Utendaji ya Shirikisho ambacho kilikaa Agosti 9,2022 jijini Arusha kimekuja na mabadiliko hayo kwa kutoa taarifa kwa familia ya michezo.

Kanuni hiyo ni pamoja na ile ya matumizi ya wachezaji wa kigeni kwenye timu moja ambapo wanaoruhusiwa kusajiliwa ni wachezaji wasiozidi 12 na wanaoruhusiwa kutumika kwenye mchezo mmoja ni wachezaji wasiozidi 12 kwenye mchezo mmoja.

Ikumbukwe kuwa awali wachezaji waliokuwa wanaruhusiwa kuanza kikosi cha kwanza walikuwa ni 8 kwenye mechi za Ligi Kuu Bara.

Kanuni hiyo ambayo imeboreshwa inaanza kutumika leo Agosti 13 kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa saa 1:00 usiku.