HAJI MANARA:NILIKUJA KAMA MSHEREHESHAJI TU

HAJI Mnara,amesema kuwa kwenye tamasha la Wiki ya Mwananchi amehudhuria pale akiwa ni MC na sio msemaji wa Yanga.

Agosti 6,2022 katika kilele cha Wiki ya Mwananchi,Manara aliibuka na kufanya sapraizi kubwa kwa mashabiki na wanachama wa Yanga.

Ikumbukwe kwamba Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF) ilitoa adhabu kwa Manara Julai 21 mwaka huu ilisema hatakiwi kujihusisha na masuala ya soka,hivyo hatakuwepo katika Tamasha la Mwananchi lakini aliibuka.

Manara aliingia uwanjani akisindikizwa na walinzi kisha akachukua jukumu la kutambulisha wachezaji na benchi la ufundi kisha akaaga akisema anaondoka kwani alialikwa kuwa mshereheshaji tu.

Baada ya utambulisho Yanga iliweza kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Vipers FC na ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Yanga 0-2 Vipers SC.