BM VITUKO KAMA VYOTE,SIKU YA TATU KAZINI

 KIUNGO wa Yanga,Bernard Morrison raia wa Ghana leo Agosti 4 inakuwa ni siku yake ya tatu ya mazoezi.

Kwa sasa yupo kambini Avic Kigamboni chini ya Kocha Mkuu Nasreddine Nabi huku kocha wa viungo akiwa ni Helmy Gueldich ambaye.

Kocha wa viungo amesema kuwa kabla ya kujiunga na timu kambini alikuwa amepewa mazoezi ya kufanya hivyo kwa sasa anaendelea na mazoezi mengine kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa 2022/23.

Akiwa kambini anatajwa kuwa mchezaji mwenye vituko vingi na utani wake ambapo neno ambalo anapenda kulitumia ni ‘Jamani Jamani nimerudi’.

Nyota huyo amerejea kwa mara nyingine akitokea ndani ya Simba ambapo mkataba wake ulimeguka msimu huu wa 2021/22.