MASTAA WATANO SIMBA WAKOSA UFUNDI WA MAKI MISRI

ZORAN Maki,Kocha Mkuu wa Simba amekosa kuona ufundi wa majembe matano ya kikosi cha Simba kambini Misri kwa kuwa walikuwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa ya Tanzania,Taifa Stars.

Ni Kened Juma,Mzamiru Yassin,Kibu Dennis,Aishi Manula na Mohamed Hussein hawataibukia Misri kwa kuwa kikosi hicho kinatarajiwa kurejea kesho kuendelea na maandalizi kuelekea Simba Day,Agosti 8.

Kipa namba moja wa Simba Manula kwa msimu wa 2021/22 alicheza mechi 21 na alifungwa mabao 11 huku akiwa amecheza mechi 11 bila kufungwa ndani ya dk 1,890.

Kened alicheza mechi 10 na kutumia dk 717 huku Mzamiru yeye alicheza mechi 22 na alitumia dk 1,407 akitupia mabao mawili na pasi mbili za mabao.

Kibu yeye alikuwa ni kinara wa kucheka na nyavu ambapo alifunga mabao 8 na pasi 4 za mabao katika mechi 21 ambazo alicheza akitumia dk 1,607 na beki Zimbwe yeye alicheza mechi 22 alifunga bao moja na kutoa pasi mbili za mabao katika dk 1,813.