ZIMEBAKI siku nane kuweza kufika Agosti 8/2022 ambayo itakuwa ni siku ya Simba Day leo Uongozi wa timu hiyo umeweza kuzindua rasmi Wiki ya Simba katika Viwanja vya Mbagala Zakhiem,Dar.
Miongoni wa waliokuwepo kwenye uzinduzi huo ambao umehudhiuriwa na mashabiki wengi wa Simba ni pamoja na Mtendaji Mkuu wa Simba,Barbara Gonzalez.
Kwa mujibu wa Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba.Ahmed Ally amesema kuwa mpango wao kwa msimu huu ni wa kipekee na watafanya mambo ya kipekee kuelekea Simba Day.
“Msimu huu tutafanya uzinduzi wa kipekee,hatujawahi kufanya tangu miaka 13 ya Simba Day,tutatoa ratiba ya Simba Wiki na kutangaza mikakati na mipango yote,pia kutakuwa na burudani za kutosha,”.
Ni Zuchu leo ametambulishwa kuwa miongoni mwa wasanii ambao wataweza kutumbuiza Simba day.