LIVERPOOL YASHINDA TAJI BAADA YA MIAKA 16

 LIVERPOOL imetwaa taji la Ngao ya Jamii baada ya kuyeyuka kwa miaka 16 bila kutwaa taji hilo.

Mara ya mwisho kuweza kutwaa taji hilo ilikuwa ni mwaka 2006 baada ya kushinda mabao 2-1 dhidi ya Chelsea.

Usiku wa kuamkia leo Julai 31 imeweza kushinda kwa mabao 3-1 dhidi ya Manchester City.

Mshambuliaji mpya wa Liverpool, Darwin Nunez alipachika bao la mwisho dk ya 90+4 kwa pasi ya Andrew Robertson na alisababisha penalti dk ya 83 raia wa Misri,Mohamed Salah aliweza kufunga.

Ilikuwa ni kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa King Power na bao la kwanza lilifungwa na Trent Alexander-Arnold dk ya 21 kwa pasi ya Salah.

City walipata bao dk ya 70 kupitia kwa Julian Alvarez ambaye aliwafanya City waamini kwamba wanaweza kupindua meza lakini mambo hayakuwa hivyo.