FAMILIA YAMUONDOA BOSI YANGA

SENZO Mbatha aliyekuwa Kaimu Mtendaji wa Yanga hataongeza mkataba mwingine wa kuendelea kuitumikia timu hiyo.

Mkataba wake unaisha leo Julai 31 na kwa mujibu wa Yanga ni kwamba Senzo hayupo tayari kuweza kuongeza mkataba mwingine kuendelea kuitumikia timu hiyo.

Saabu ya yeye kuondoka Yanga ni masuala ya kifamilia hasa kuwa mbali nayo kwa muda akiwa nchini Tanzania jambo ambalo limemfanya asiongeze mkataba mwingine ndani ya Yanga. kwa kuwa familia yake ipo Afrika Kusini.

Kikao ambacho kilijadili masuala ya Yanga ambacho kilikutana jana Hotel ya Serena licha ya kuweza kumuomba abaki mambo yalikuwa tofauti.

Ni wakili Simon Patrick atakuwa ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Yanga wa mpito.