TIMU ya Taifa ya Tanzania,Taifa Stars leo imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Somalia ikiwa ni mchezo wa kuwania kufuzu CHAN.
Mabao ya Tanzania yamefungwa na Abdul Suleiman dk 33 na Dickson Job dk ya 67.
Mchezo wa leo umechezwa Uwanja wa Mkapa ambapo Stars ilianza kufunga kipindi cha kwanza kupitia kwa Sopu ambaye amekuwa kwenye mwendo mzuri ndani ya Stars.
Kipindi cha pili yamepatikana mabao mawili ambapo walianza Somalia huku mtupiaji akiwa ni Farhan Ahmed dk 47 ya mchezo huo ikiwa ni mwanzo kabisa wa kipindi cha pili.
Job aliweza kufunga mabao kwa mkwaju wa penalti ambao umesababishwa na Sopu aliyechezewa ndani ya 18.
Stars inasonga mbele na inatarajiwa kucheza na Uganda mchezo ujao ikiwa imeweza kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-1.