JEMBE:TARIMBA HAHUSIKI SIMBA KUJIONDOA SPORTPESA

MCHAMBUZI wa soka nchini Saleh Ally Jembe ametoa ufafanuzi kuhusu taarifa zinazoenea mitandaoni kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa SportPesa Abas Tarimba amehusika katika kukwamisha dili la Kampuni hiyo yakubashiri na Simba SC.

Jembe amesema habari hizo si za kweli licha ya kwamba Tarimba ni mwana Yanga lakini Simba waliachana na dili la SportPesa kutokana na kupata dili jingine la M- Bet

Aidha amesisitiza kuwa Tarimba ndiyo alikuwa mtu wa kwanza kuvishawishi vilabu hivi vikubwa nchini vya Yanga na Simba kukubali udhamini wa SportPesa mwaka 2017 ili kuvisaidia viweze kujiendesha kwa mafanikio na ni katika kipindi hicho ambapo Simba SC imepata mafanikio makubwa licha ya kuwa ilikuwa inapaka mkataba wenye maslahi sawa na watani wao wa jadi Yanga SC.

Julai 27,2022 Klabu ya Yanga ilisaini mkataba na Kampuni ya Michezo ya kubashiri ya SportPesa wenye thamani ya zaidi ya Bilioni 12 za kitanzania ambao utadumu kwa muda wa miaka mitatu (3).