ALIYEKUWA Kocha Mkuu wa Al Ahly ya Misri, Pitso Mosimane raia wa Afrika Kusini ameitikia ombi la Klabu ya Yanga na kuthibitisha kuwa atahudhuria katika wiki ya Mwananchi itakayofanyika Agosti 6, 2022 jijini Dar es Salam.
Ikumbukwe kuwa, Juni 26, 2022, Pitso aliipongeza Yanga kwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya NBC na kufanyiwa gwaride la heshima huku akisema kuwa Afrika nayo inaweza kufanya magwaride yao ya Ubingwa kama Ulaya.
Pitso aliongeza kuwa angetamani kuja Tanzania kutazama mechi ya Yanga SC na Coastal Union fainali ya FA lakini majukumu yalimbana akaomba link ya kutazama mechi hiyo.
Hata hivyo aliomba kujua Ratiba ya Simba na Yanga ili kuja Tanzania kuutazama mchezo huo.
Mazungumzo yake na Rais wa Yanga, Injinia Hersi kupitia twita yameonesha kwamba amekubali kuweza kuja kwenye wiki ya Mwananchi ambayo hutumika kuweza kufanya utambulisho wa wachezaji wapya pamoja na uzi ambao utatumika kwa msimu wa 2022/23.