UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa hesabu kubwa ni kukusanya mataji yote matatu iliyotwaa kwa msimu wa 2021/22.
Ni Ngao ya Jamii Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho ambayo waliyatwaa msimu uliopita yote yalikuwa mikononi mwa Simba hivyo wanakazi ya kuweza kuyatetea kwa mara nyingine tena.
Kaimu Mtendaji wa Simba,Senzo Mbatha amesema kuwa wanatambua kwamba msimu ujao utakuwa na ushindani mkubwa ambapo kila timu inahitaji kupata matokeo chanya.
“Tunajua kwamba msimu ujao utakuwa na ushindani mkubwa hasa katika kutetea mataji yetu na tutaanza na Ngao ya Jamii dhidi ya Simba hapo tuna kazi ya kufanya lakini tupo tayari na tunahitaji taji hilo.
“Kila mmoja anajua kwamba haikuwa kazi rahisi kuweza kutwaa haya mataji lakini ni furaha kwa kila mmoja hasa baada ya kukamilisha msimu tukiwa na mafanikio haya,”
Zimebaki siku 20 kabla ya watani wa jadi Yanga na Simba kuweza kucheza kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.