MCHEZO wa pili wa kirafiki kwa washindi namba mbili wa Ligi Kuu Bara Simba uliochezwa usiku wa kuamkia leo nchni Misri ilikuwa dhidi ya Al Akkhood Club ya Misri na Simba kuibuka na ushindi mkubwa.
Ilikuwa ni ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Al Akhdood Club ya Misri ambapo Kocha Mkuu Zoran Maki aliweza kuongoza kikosi chake kilichaoanza langoni na Ally Salim kipa namba tatu wa Simba.
Baada ya ushindi huo Simba wameabinisha kuwa walikuwa wanamsubiri kwa hamu kocha huyo Maki ambaye ni kocha wa ushindi.
Watupiaji kwenye mchezo huo walikuwa ni Moses Phiri kwa pasi ya Clatous Chama,Jonas Mkude kwa pasi ya Okra,Meddie Kagere kwa pasi ya Banda,Sakho alitupia mabao mawili na pasi moja alipewa na Banda na mwingine ni Erasto Nyoni naye alitupia bao moja.
Mchezo wa kwanza Simba wa kirafiki ilicheza dhidi ya Ismailia ya Misri.
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally ameweka wazi kuwa wanazidi kujiimaraisha kwa ajili ya msimu ujao wa 2022/23