KIBAYA NI MALI YA IHEFU FC

JAFARY Kibaya nyota aliyekuwa anakipiga ndani ya Mtibwa Sugar sasa ni mali ya Ihefu FC ya Mbeya baada ya kutambulishwa jana Julai 22,2022.

Nyota huyo anakuwa miongoni mwa nyota wa mwanzo kutangazwa kwenye timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu,Zuber Katwila.

Kibaya amesema:”Ni muda wa kutoa shukran zangu za dhati kwenu hakika mlinilea na kunikuza vizuri kwenye wakati wote ambao nilikua hapo siwezi kusahau ila shukrani sana kwa yoye na niwatakie muendelezo mwema wa mapambano ya ligi na mwenyezi Mungu awaepushie misukosuko ya hapa na pale.

Ofisa Habari wa Ihefu FC,Andrew Peter ameweka wazi kuwa wanahitaji kuboresha kikosi hicho ili kuleta ushindani kwa msimu ujao wa 2022/23.

Mchezaji mwingine ambaye ametambulishwa ndani ya Ihefu FC ni Peter Mwalianzi