WAKATI wa maandalizi kwa ajili ya msimu mpya kwa sasa ni lazima yaanze hasa ukizingatia kwamba Agosti ni ligi inatarajiwa kuanza.
Ukweli ni kwamba kwa sasa wapo ambao wapo kambini na wengine hawajaanza kambi yote ni mipango ambayo inawekwa na kila mmoja ambaye ni kiongozi.
Acha hayo kuna suala limekuwa lizizungumzwa kuhusu wapi kambi inapaswa kuwekwa kwa msimu wa 2022/23.
Hapa ni muda wa kujua ni ndani ya Tanzania ama nje ya Tanzania kila mmoja ana wajibu wa kufanya maamuzi sahihi na sio kupewa shinikizo kutoka kwa mashabiki ama timu fulani kuweka kambi mahali fulani.
Benchi la ufundi ni muda wa kutazama na kujua wapi wanahitaji kuweka kambi ambayo inaendana na mazingira ya Tanzania hasa ukizingatia kwamba ligi inachezwa hapahapa na sio nje ya nchi.
Mazingira ya Tanzania kuna sehemu nzuri na bora kwa ajili ya kuweka kambi hilo linawezekana kwa kufanya uchaguzi mzuri.
Kila kitu pia kipo hapa Tanzania ikiwa ni pamoja na viwanja na sehemu za kufanyia mazoezi yaani GYM ni chaguo la wahusika kuweka wazi kwamba wanahitaji kwenda wapi.
Kuna wale ambao wanashindwa kuelekea nje ya nchi kutokana na suala la uchumi kwani kila timu ina bajeti yake hivyo hakuna haja ya kuweza kuwapangia watu sehemu ya kuweka kambi.
Iwe Tanzania ama nje ya Tanzania kambi lazima ifuate mipango ya benchi la ufundi na iwe inalingana na mazingira halisi ya Tanzania.
Kikubwa ni mpangilio wa kile ambacho kinahitajika hasa uhakika wa sehemu za mazoezi na sehemu ya kupumzika.
Uimara wa wachezaji katika kuchukua mafunzo wanayopewa na walimu itawafanya waweze kupata kile ambacho ni bora kwao na itawajenga waweze kuanza msimu kwa kasi.
Makosa ambayo yalifanywa msimu uliopita kwenye maandalizi yasipewe nafasi kwa kuwa matokeo ya mechi ambazo huwa zinachezwa ni maandalizi.
Kila kitu kwenye mchezo wa mpira ni maandalizi na ikumbukwe kwamba wakati ule uliopita kila timu ilikuwa inatamba kufanya maandalizi mazuri.
Muda ni mchache lakini matumizi mazuri ya muda huu yatakuwa ni faida kwa kila mmoja ambaye ataweza kuutumia kwa faida.
Yote kwa yote kuelekea kwenye msimu mpya wa 2022/23 basi wakati wa kubadili mtazamo na majina yakuwaita wachezaji wetu wazawa.
Imekuwa kawaida kuona kwamba majina ya wachezaji wakigeni ni yale yenye picha nzuri na inayovutia hasa kwa kila anayeitwa.
Lakini inapofikia kwa wachezaji wazawa wengi wamekuwa wakipewa majina ambayo hayaleti picha nzuri ila wakati mwingine yamekuwa hayaleti maana bora.
Unaona kwamba mchezaji anapewa jina la kiungo punda na yeye anafanya kazi ya kuipeperusha bendera ya Tanzania.Kubadili kwa majina ya hawa wachezaji kutawafanya waweze kuongeza juhudi na kufanya kazi ambayo itawafanya waweze kuongeza juhudi zaidi na zaidi.