AZAM FC KUWEKA CHIMBO LA SIKU 20 MISRI

Kikosi cha Azam FC leo Julai 22 kimeelekea Misri kwa ajili ya kambi ya maandalizi ya Ligi Kuu Bara pamoja na mashindano mengine ikiwa ni pamoja na Kombe la Shirikisho na kitaweka kambi jijini El Gouna, Misri kwa siku 20.

Kabla ya kukwea pia kuelekea Misri Azam FC wao walianza kambi ya ndani kwa ajili ya kujiweka fiti kwa mazoezi ambayo walikuwa wanatumia Uwanja wa Azam Complex.

Mpango kazi ulikuwa ni kwenye gym pamoja na mbinu za uwanjani kwa kupeana maufundi kupitia kwa Kocha Mkuu Abdihamid Moallin.

Kocha huyo ameweka wazi kwamba anaamini kwa namna ambavyo vijana wake wamekuwa wakijituma watakuwa kwenye ubora msimu ujao na kambi itakuwa na manufaa kwao.

“Tunatambua kwamba kwa sasa ni maandalizi ya msimu mpya hilo linatufanya tuweze kuwapa mbinu vijana kwa ajili ya kuwa imara.

“Miongoni mwa program ambazo waliweza kufanya ni pamoja na mazoezi ya utimamu wa mwili,kuwaweka sawa kisaikolojia pamoja na mazoezi ya uwanjani,”.

Kwenye msafara huo miongoni mwa wazawa ambao walikuwa nje kwa muda kutokana na kutiu majeraha ni pamoja na Idd Suleiman,’Nado’ ambaye yupo kwenye msafara.

Wengine ni pamoja na Ibrahim Ajibu,Idris Mbombo,Rodgers Kola.Shaban Chilunda,Prince Dube na Ibrahim Ajibu.