SAKHO BAO LAKE LAINGIA TATU BORA CAF

KIUNGO wa Simba Pape Sakho bao lake limeingia kwenye tatu bora kwa wale ambao wanaowania tuzo ya bao bora la CAF msimu wa 2021/22.

 Kwa hatua hiyo bao la nyota huyo anayekipiga ndani ya Simba limepigiwa kura kiasi kikubwa na mashabiki wa Sakho ambao ni Watanzania pamoja na mashabiki wa mpira waliopo Tanzania na nje ya Tanzania.

Tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa kesho Julai 21 hivyo mbivu na mbichi zitajulikana kwa nani atakayesepa na bao bora.

Bao hilo alipachika kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Uwanja wa Mkapa mbele ya ASEC Mimosas na Simba ilishinda mabao 3-1.

Mwingine mtupiaji anayewania tuzo hiyo ni Zouhair El-Moutaraji  alifunga kwenye mchezo wa Wydad vs Al Ahly na Gabadinho Mhango mchezo wa Malawi vs Morocco.

Mpigie kura Sakho kupitia http://cafawards2022-goty.com