GEORGE MPOLE YUPO SANA GEITA GOLD

 GEORGE Mpole mtupiaji namba moja ndani ya ligi msimu wa 2021/22 baada ya kufunga mabao 17 huenda akasalia ndani ya Geita Gold.

Awali alikuwa anatajwa kuibuka ndani ya timu zilizomaliza tatu bora kwa ajili ya kuwa hapo msimu wa 2022/23.

Kocha wa Geita Gold,Felix Minziro aliwahi kusema kuwa kutokana na kiwango ambacho amekionyesha mchezaji huyo aliweza kuwa sokoni kwani ni mchezaji mzuri.

Kwenye usiku wa mastaa nyota huyo alipewa tuzo ya mfungaji bora na alikuwa kwenye orodha ya wachezaji waliopo kikosi bora msimu wa 2021/22.

  Vigogo Yanga,Simba na Azam FC hawa walikuwa wakitajwa kuwania saini yake ila mpaka sasa timu hizo zimekamilisha usajili kwa asilimia kubwa.

Azam FC wao wamefunga usajili wao kwa kuwasajili nyota tisa ambapo wazawa ni watatu na wachezaji wakigeni ni 6.