WIKI YA MWANANCHI KUANZA AGOSTI MOSI

WIKI ya Mwananchi itaanza rasmi Agosti Mosi mwaka huu wa 2022 ambapo wanatarajia kucheza mchezo na timu ya kimataifa Uwanja wa Mkapa.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Haji Manara amebainisha kwamba kambi ya maandalizi kwa msimu wa 2022/23 inatarajiwa kuanza kesho Julai 20,2022 Kigamboni.

“Tutafanya kambi yetu Kigamboni ambapo kuna eneo zuri na tulivu kwa ajili ya wachezaji kuweza kupata muda wa kufanya maandalizi ya msimu mpya na ni lazima tufanye maandalizi mazuri.

  “Kuhusu Mwananchi Day tutaanza Agosti Mosi na kilele chake itakuwa ni Agosti 6. Itakuwa ni wiki ya kipekee na itakuwa special (maalumu) na bora sana kuliko zote zilizopita.

” Mwisho kabisa tuko tayari kwa maandalizi ya msimu ujao na tunaamini kwamba kila kitu kitakuwa sawa na tutafanya vizuri,” amesema Manara.