TAIFA STARS WAANZA MAZOEZI

WACHEZAJI  wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars wameanza maandalizi kwa ajili ya michezo ya kufuzu CHAN 2023.

Stars inayonolewa na Kocha Mkuu,Kim Poulsen inatarajiwa kucheza mechi mbili ndani ya mwezi huu wa Julai kuwania kufuzu CHAN.

Itakuwa mchezo dhidi ya Somalia ambapo ule wa awali unatarajiwa kuchezwa Julai 23 na ule wa pili unatarajiwa kuchezwa Julai 30,2022 katika Uwanja wa Mkapa.

Leo Julai 16,2022 Taifa Stars imeanza mazoezi kwenye uwanja wa Uhuru kujiandaa na michezo hiyo muhimu.

Miongoni mwa mastaa ambao walikuwa kwenye kikosi ni pamoja na Aishi Manula,Metacha Mnata,Kennedy Juma,Relliats Lusajo,Abdul Suleiman,’Sopu’.