>

KIUNGO YANGA AINGIA ANGA ZA SINGIDA BIG STARS

BAADA ya mabosi wa Yanga kumpa mkono wa kwa kheri nyota wao Deus Kaseke Julai 14 inaelezwa kuwa nyota huyo yupo kwenye mazungumzo na Singida Big Stars ili aweze kuwa ndani ya timu hiyo kwa msimu ujao wa 2022/23.

 Taarifa rasmi iliyotolewa na Yanga iliweka wazi kwamba; “Umekuwa sehemu kubwa ya mchango wa mafanikio kwenye Klabu yetu, tunakutakia kila la kheri na mafanikio uendako.”

Kwa upande wake, Kaseke kupitia ukurasa wake wa Instagram ameishukuru Yanga kwa kipindi chote ambacho ameitumikia. kwa kuandika ujumbe:-“Asante sana Yanga mmekuwa sehemu kubwa saana ya maisha yangu ya mpira, nashukuru kwa sapoti kubwa mlionipa kipindi chote nilichotumikia Timu ya Wananchi, asanteni sana Wananchi.

Kaseke ameitumikia klabu hiyo kwa muda wa zaidi ya miaka mitano akishinda mataji mawili ya Ligi Kuu Tanzania Bara.