COASTAL Union wameanza na kuongeza nguvu kwenye ulinzi baada ya Julai 14,2022 kukamilisha usajili wa mlinda mlango namba mbili wa timu ya Taifa ya Comoro, Mahamoud Mroivili.
Unakuwa ni usajili wa kwanza ndani ya Coastal Union inayonolewa na Kocha Mkuu, Juma Mgunda.
Kipa huyo amepewa dili la miaka miwili kuweza kuitumikia timu hiyo kwa ajili ya msimu wa 2022/23.
Ikumbukwe kwamba Coastal Union ni mabingwa wa pili ndani ya Kombe la Shirikisho ambapo waliweza kugotea kwenye fainali na kupoteza kwa kufungwa na Yanga kwa penalti 4-1 baada ya dk 120 kukamilika kwa kufungana mabao 3-3.
Ataungana na kipa namba moja wa Coastal Union ambaye ni Mussa Mbissa aliyewahi kucheza Mwadui FC na Yanga Junior