>

USIKU WA MANANE YANGA WAMTAMBULISHA WINGA WA KAZI

 RASMI Yanga imefanikiwa kupata saini ya winga wa kimataifa wa Burkina Faso, Aziz Ki ambaye ametambulishwa usiku wa kuamkia leo Julai 15, 2022.

NI usiku wa manena nyota huyo winga wa kazi aliyewapa tabu Simba kwenye mashindano ya kimataifa aliweza kutamulishwa rasmi.

Nyota  huyo ametokea Klabu ya ASEC Mimosas inayoshirki Ligi Kuu ya Ivory Coast ambapo usajili wake ulivuta hisia za wengi.

Awali alikuwa anatajwa kuingia kwenye rada za Simba na Azam FC kisha mabosi wa Yanga wakamfuata jumlajumla na kumalizana naye.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Haji Manara amesema kuwa wale ambao walikuwa wanawabeza kuhusu kuipata saini ya nyota huyo sasa watakuwa wanaona vitendo.

“Kwa wale ambao walikuwa wanabeza kwamba hatuwezi kupata saini ya nyota mwenye uwezo mkubwa na namba 10 bora basi iwafikie kwamba tumempata na tupo naye ndani ya kikosi cha Yanga,” .

Ni kandarasi ya miaka miwili nyota huyo amesaini ndani ya kikosi cha Yanga ambao ni mabingwa wa ligi msimu wa 2021/22.