UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa kwa namna ambavyo wanasajili wachezaji wenye uwezo mkubwa wapinzani wao watasubiri kuwashusha hapo walipo kwa sasa.
Yanga imeweza kumalizana na nyota wa kazi ikiwa ni pamoja na kiungo Bernard Morrison,Lazarus Kambole na Gael Bigirimana ambao wana uhakika wa kuwa kwenye kikosi hicho msimu ujao.
Ofisa Habari wa Yanga, Haji Manara amesema kuwa kazi ambayo wataifanya uwanjani itakuwa kubwa na itawapa tabu wapinzani kuwashusha.
“Kwa usajili ambao tunaufanya na malengo makubwa ambayo tunayo kwa wapinzani wetu itakuwa ngumu kutushusha hapa tulipo hivyo wajipange kwa wakati mwingine.
“Hatuna utani tumemaliza ligi kwa mafanikio makubwa ambapo awali walikuwa wanabeza mipango yetu lakini yote yameonekana tumemaliza ligi bila kufungwa,sasa tunakwenda kuweka historia nyingine kwa msimu ujao,” amesema