>

SIMBA:WACHEZAJI WAZAWA KWETU WANASIMAMISHA NCHI

 UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa usajili wa wachezaji wazawa ndani ya kikosi hicho ni usajili wa kuweza kusimamisha nchi kwa kuwa kila mchezaji ana thamani kubwa.

Tayari Simba imetambulisha wachezaji wawili wazawa kwa ajili ya msimu ujao ikiwa ni pamoja na Habib Kyombo aliyekuwa anakipiga ndani ya Mbeya Kwanza na Nassoro Kapama ambaye alikuwa anacheza ndani ya Kagera Sugar.

Mkuu wa Kitengo cha Habari ndani ya Simba, Ahmed Ally ameweka wazi kuwa kila aina ya usajili ambao unafanywa ni bora na kwa manufaa ya timu bila kujali wapi ambapo anatokea.

“Ikiwa unazungumzia wachezaji wazawa kwetu ni usajili mkubwa na wa viwango ambao unasimamisha kabisa nchi kwani hawa ni wachezaji wazuri na wanakuja Simba kufanya mambo mazuri kwa ajili ya Watanzania na mashabiki wake.

“Tunawaheshimu wachezaji wazawa kwa kuwa wanajituma na sio kwa ajili ya Simba bali kwa taifa kwa kuwa wanapata nafasi kucheza mechi za kimataifa pamoja na kucheza timu ya taifa,” amesema.