>

MANZOKI,MNIGERIA WAINGIA ANGA ZA SIMBA

MASTAA watatu wa kimataifa wanatajwa kuwa kwenye hesabu za Simba ambayo jana ilimtambulisha nyota mpya ambaye Nassoro Kapama kutoka Kagera Sugar.

Kapama yeye ni mzawa amepewa dili la miaka miwili kwa ajili ya kuwa ndani ya timu hiyo.

Cesar Manzoki huyu ni raia wa Uganda kwa ajili ya kuongeza nguvu ndani ya kikosi hicho na Nelson Okwa raia wa Nigeria.

Agustine Okrah raia wa Ghana ambaye ni winga mwenye uwezo wa kupanda na kushuka.

Mmoja kati ya hao anatarajiwa kutambulishwa hivi karibuni baada ya kukamilisha kusaini dili la miaka miwili.