>

JOYCE LOMALISA NI NJANO NA KIJANI,ASAINI DILI KWA MABINGWA

JOYCE Lomalisa ni nyota mpya ndani ya kikosi cha Yanga baada ya kutambulishwa usiku wa kuamkia leo Julai 12,2022 na mabosi wa timu hiyo ambayo imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2021/22.

  Yeye ni beki raia wa DR Congo kwa dili la miaka miwili ambapo alikuwa akicheza Klabu ya Bravaso do Maqui na amewahi kucheza pia Klabu ya Interclub ya nchini Angola.

Malengo ya Klabu ya Yanga ni kuhakikisha kwamba wanaweza kufanya vizuri kimataifa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo watashiriki msimu huu wa 2022/23 baada ya kutwaa ubingwa wa ligi.

Kwa mujibu wa Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said amebainisha kwamba malengo ya timu hiyo ni kufanya vizuri kwenye ligi za ndani na za nje pia.