>

AZAM FC KUKWEA PIPA MPAKA MISRI

 JULAI 22,2022 kikosi cha Azam FC kinatarajiwa kuondoka Dar na kuibukia nchini Misri kwa ajili ya kuweka kambi kwa maandalizi ya msimu wa 2022/23 watakaa huko hadi Agosti 12,2022 kwenye Mji wa El Gouna,

Kwa Mujibu wa Ofisa Habari wa Azam FC,Zakaria Thabit amebainisha hayo kwa kuweka wazi kuwa hayo yametokea baada ya vikao kuweza kujadiliwa.

Ikumbukwe kwamba tayari Azam FC imeweza kutambulisha nyota wake wapya ambao watakuwa kwenye kikosi hicho kwa msimu mpya ujao wa 2022/23.

Miongoni mwa nyota ambao wapo kwenye kikosi cha Azam FC ni pamoja na Nathaniel Chilambo,Cleophance Mkandala,Kipre Junior,Tape Edinho,Isah Ndala na Abdul Suleiman.

Wachezaji wanatarajia kuingia kambi ya Dar Julai 15.17 2022 na Julai 18 wataanza mazoezi kabla ya kuanza safari ya kwenda Misri.