METACHA MNATA NI SINGIDA BIG STARS

RASMI Metacha Mnata ni mali ya Singida Big Stars ambayo imepanda Ligi Kuu Bara msimu huu ikitokea Championship.

Julai 10,2022 Singida iliweza kumtambulisha nyota huyo kwa kubainisha kwamba atakuwa ni mchezaji wao rasmi.

Mnata alikuwa ndani ya Polisi Tanzania kwa msimu uliopita wa 2021/22 ambapo aliweza kukusanya jumla ya clean sheet 8.

Hussein Masanza, Ofisa Habari wa Singida Big Stars amesema kuwa kipa huyo amewahakikisha kwamba atafanya kazi kubwa lango kuweka ulinzi.

“Ni mlinzi imara na amekuwa akifanya vizuri hata anapokuwa kwenye timu ya Taifa ya Tanzania,Taifa Stars, Metacha Mnata, ametuhakikishia kuwa lango letu litakuwa salama kupitia uzoefu wake.

“Tayari tumeinasa saini yake na atakuwa nasi kwa mkataba wa miaka miwili katika nafasi ya mlinda mlango,” .