>

KAPAMA RASMI NI SIMBA

 NASSORO Kapama ni nyota mpya wa Simba akiwa ametambulishwa leo Julai 11,2022

Kapama ni mzawa wa pili kutambulishwa ndani ya kikosi cha Simba baada ya kuanza na Habib Kyombo ambaye alikuwa anakipiga ndani ya Mbeya Kwanza.

Nyota huyu alikuwa anacheza Kagera Sugar msimu wa 2021/22 hivyo msimu wa 2022/22 atakuwa ndani ya kikosi cha Simba.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano ndani ya Simba,Ahmed Ally amebainisha kuwa wataleta wachezaji wazuri.

“Tunafanya usajili mzuri kwa ajili ya msimu ujao na hilo lipo wazi kikubwa ni mashabiki wasiwe na mashaka kuhusu kazi ambayo tunaifanya kwa sasa,”.